Skip to main content

Posts

 Klabu ya Yanga SC imetambulisha usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka Zoman FC, Celestin Ecua (23), ambaye msimu uliopita aliitumikia ASEC Mimosas kwa mkopo. Katika msimu wake wa mwisho akiwa ASEC Mimosas, Ecua alionyesha kiwango cha juu kwa kufunga mabao 15 na kutoa assists 12 katika michuano yote  Ni takwimu ambazo si tu zinaashiria uwezo wake wa kumalizia, bali pia ubunifu wake katika kutoa pasi za mabao.
Recent posts

DUKE ABUYA AONGEZA MKATABA YANGA

 Katika kipindi hiki cha dirisha la usajili, klabu ya Yanga SC imeendelea kudhihirisha ukubwa wake si kwa kusajili majina mapya tu, bali kwa kuhakikisha inawadhibiti nyota wake muhimu waliokuwa wamemaliza mikataba. Hili limekuwa ni jambo la msingi kwa timu kubwa duniani, kuimarisha misingi kabla ya kuongeza mapambo.Baada ya kuthibitisha kuwaongezea mikataba Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua, sasa ni rasmi kuwa kiungo mahiri kutoka Kenya, Duke Abuya, ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga kwa misimu miwili mingine. Abuya ni mmoja wa wachezaji waliotoa mchango mkubwa katika mafanikio ya Yanga msimu uliopita. Katika nyakati ambazo Yanga ilimkosa kiungo mkabaji Khalid Aucho, Abuya alionyesha ubora mkubwa kwa kuimarisha eneo hilo na kushirikiana kwa ustadi na wachezaji wenzake kama Mudathir na Maxi Nzengeli  Inaonekana wazi kuwa uamuzi wa Yanga kutomuongezea mkataba Khalid Aucho umechochewa na kiwango cha kuaminika alichokionyesha Abuya. Uwezo wake wa kutimiza majukumu kati...

Taifa star yailaza senegali 2_1

 Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeendelea kufanya vizuri katika mashindano ya CECAFA ya Mataifa Matatu kwa kuichapa Senegal mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Dimba la Black Rhinos, Karatu, Tanzania. Timu ya Taifa ya Senegal walianza kupata bao mapema dakika ya 8’ kupitia kwa Mapathe Mbodji, na baadae Stars wakafanya ‘Comeback’ kupitia kWa Abdul Sopu 53’ (P) na Ibrahim Hamad Bacca 56’ akafunga goli la ushindi. Timu ya Taifa ya Senegal walianza kupata bao mapema dakika ya 8’ kupitia kwa Mapathe Mbodji, na baadae Stars wakafanya ‘Comeback’ kupitia kWa Abdul Sopu 53’ (P) na Ibrahim Hamad Bacca 56’ akafunga goli la ushindi. Ikumbukwe Tanzania imeshinda mechi zote mbili na kuondoka na Karatu na alama sita. Mchezo wa kwanza walishinda 1-0 dhidi ya Uganda.