Katika kipindi hiki cha dirisha la usajili, klabu ya Yanga SC imeendelea kudhihirisha ukubwa wake si kwa kusajili majina mapya tu, bali kwa kuhakikisha inawadhibiti nyota wake muhimu waliokuwa wamemaliza mikataba. Hili limekuwa ni jambo la msingi kwa timu kubwa duniani, kuimarisha misingi kabla ya kuongeza mapambo.Baada ya kuthibitisha kuwaongezea mikataba Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua, sasa ni rasmi kuwa kiungo mahiri kutoka Kenya, Duke Abuya, ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga kwa misimu miwili mingine.
Abuya ni mmoja wa wachezaji waliotoa mchango mkubwa katika mafanikio ya Yanga msimu uliopita. Katika nyakati ambazo Yanga ilimkosa kiungo mkabaji Khalid Aucho, Abuya alionyesha ubora mkubwa kwa kuimarisha eneo hilo na kushirikiana kwa ustadi na wachezaji wenzake kama Mudathir na Maxi Nzengeli
Inaonekana wazi kuwa uamuzi wa Yanga kutomuongezea mkataba Khalid Aucho umechochewa na kiwango cha kuaminika alichokionyesha Abuya. Uwezo wake wa kutimiza majukumu katika eneo la kati umeipa Yanga uhakika mpya.
Baada ya kuthibitisha kuwaongezea mikataba Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua, sasa ni rasmi kuwa kiungo mahiri kutoka Kenya, Duke Abuya, ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga kwa misimu miwili mingine.
Kuendelea kwa Abuya ndani ya timu ni kama usajili mpya wenye thamani kubwa, ukizingatia kuwa amezoea mfumo wa Yanga, anaelewana vyema na wachezaji wenzake, na tayari amethibitisha uwezo wake kwenye mashindano ya ndani na ya kimataifa.
Yanga SC inaonyesha kwa vitendo dhamira ya kuendeleza mafanikio yake kwa kutegemea msingi imara wa wachezaji waliokwisha kuonyesha thamani yao. Kuongeza mkataba wa Abuya ni hatua sahihi, ya kimkakati na yenye faida kubwa kwa klabu msimu ujao.
Comments
Post a Comment