Klabu ya Yanga SC imetambulisha usajili wa kiungo mshambuliaji kutoka Zoman FC, Celestin Ecua (23), ambaye msimu uliopita aliitumikia ASEC Mimosas kwa mkopo. Katika msimu wake wa mwisho akiwa ASEC Mimosas, Ecua alionyesha kiwango cha juu kwa kufunga mabao 15 na kutoa assists 12 katika michuano yote Ni takwimu ambazo si tu zinaashiria uwezo wake wa kumalizia, bali pia ubunifu wake katika kutoa pasi za mabao.